Korea Kaskazini yaipa onyo kuishambulia Marekani na makombora ya kinyuklia

Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia msha...

Korea Kaskazini imeionya Marekani kutoanzisha vitendo vya uchokozi katika eneo la Korea ikisema kuwa iko tayari kulipiza kisasi kupitia mshambulio ya kinyuklia. Taifa hilo limesema hivyo wakati ambapo kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, amehudhuria gwaride la heshima katika mji mkuu wa Pyong yang, akiadhimisha siku ya kuzaliwa ya babu yake, marehemu Kim II-Sung, ambaye ni mwanzilishi wa taifa hilo.

"tumejiandaa kwa vita kamili'' ,alisema Choe Ryong-hae, anayeaminika kuwa mu wa pili mwenye uwezo mkubwa katika taifa hilo.''Tuko tayari kulipiza kisasi na mashambulio ya Nuklia kwa mbinu zetu dhidi ya shambulio lolote la Kinyuklia''.Huku kukiwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inakaribia kupata ufanisi wa kukamilisha silaha za Kinyuklia, Gwaride la Jumamosi ilikuwa fursa kwa bwana Kim kuonyesha uwezo wa kijeshi wa taifa hilo.

Vifaa vilivyoonyeshwa kwa mara ya kwanza vilikuwa vilevilivyotajwa kuwa manuwari za Pukkuksong,makombora ya masafa marefu yanayoweza kwenda kwa takriban kilomita 1000.Wachanganuzi wa vifaa vya kijeshi pia wanasema kuwa kuna makombora mawili mapya yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine, lakini haijulikani iwapo yamefanyiwa majaribio.

Kulikuwepo na sherehe za kawaida, kama vile mamia yawanajeshi kupiga gwaride na msafara wa magari ya kivita huku yakiwa yamebeba silaha kama vile makombora.Maonyesha ya silaha nyingi yanaendelea nchini humo wakati ambapo kuna hali ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani kufuatia mazoezi ya makombora ya kinyukilia yanayoandaliwa na Korea Kaskazini.Hali ya wasiwasi imekumba eneo la Korea kwa ujumla kufuatia majaribio kadhaa ya makombora ya kisasa na Korea Kaskazini na mapema Jumamosi shirika la habari la taifa hilo lilionya Marekani kusitisha kiherehere chake cha vitisho vya kijeshi.Marekani imetuma meli kadhaa za kivita katika Rasi ya Korea.Hiyo jana waziri wa mashauri ya kigeni wa Uchina alionya kuwa vita vyovyote kati ya Korea Kaskazini na Marekani havitamfaidi ye yote.


COMMENTS

Name

kimataifa,1,Mlipuko,1,mtandao,1,teknolojia,1,
ltr
item
BONGO DONE: Korea Kaskazini yaipa onyo kuishambulia Marekani na makombora ya kinyuklia
Korea Kaskazini yaipa onyo kuishambulia Marekani na makombora ya kinyuklia
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3yUvwAuxn1lu4-N_ordT3Xzm9VnrcgHqjFdY-o3lZUWm1s7equJD3VRgZ47HH-hoV2IXd9VmjB5U1X-Uigj0-BhgCqjWD2Hi6WYpWU2-wccXnwrjtquhmFohj-nnfXTTEXcTNw9PD478b/%20cursor:%20pointer;
BONGO DONE
https://bongodone.blogspot.com/2017/04/korea-kaskazini-yaipa-onyo-kuishambulia.html
https://bongodone.blogspot.com/
https://bongodone.blogspot.com/
https://bongodone.blogspot.com/2017/04/korea-kaskazini-yaipa-onyo-kuishambulia.html
true
5217992609549716446
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy