Sasa ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji

Kampuni ya simu za mkononi nchini Vodacom Tanzaniaitakuwa kampuni ya kwanza inayotoa huduma za mawasiliano kuuza hisa zake katika soko la hi...

Kampuni ya simu za mkononi nchini Vodacom Tanzaniaitakuwa kampuni ya kwanza inayotoa huduma za mawasiliano kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam maarufu kama DSE.

Hii inafuatia rasimu ya waraka wa matarajio (Prospectus) na maombi yaliyotumwa kwenye Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kukubaliwa.

CMSA ndiyo mamlaka inayosimamia masoko ya mitaji na dhamana nchini.Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Ian FerraoUuzaji wa hisa za awali wa Vodacom Tanzania Limited PLC ni katika utekelezaji wa Sheria ya Posta na Mawasiliano iliyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha mwaka 2016 ambayo inaagiza kampuni zote za simu za mikononi kuuza 25% ya hisa zao kwa umma.

Hisa za kampuni hiyo inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi zaidi nchini, huenda sasa zikaanza kuuzwa muda wowote kuanzia wiki hii au wiki ijayo.

Vodacom Tanzania inatarajia kuorodhesha asilimia 25 ya hisa zake katika soko la mitaji ambayo ni sawa ni hisa milioni560 zitakazokuwa na thamani ya shilingi bilioni 476 huku kila hisa ikiuzwa kwa Tsh 850.

Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom Tanzania ikizingatiwa kwamba kampuni nyingine za simu zinasuasua. Vodacom inatarajiwa kuwa miongoni mwa kampuni zitakazokuwa na mitaji mikubwa katika soko la DSE.

Kampuni nyingine zenye mitaji mikubwa ni Acacia, EABL na TBL. Hadi hivi sasa DSE ina kampuni 25 zilizoorodheshwa ambapo kampuni za ndani ni 18 na zile zilizoorodheshwa kutoka masoko ya kigeni yakiwemo London na Nairobi ni 7.

Taarifa rasmi za mauzo ya awali ya hisa hizo milioni 560lini zitaanza kuuzwa, na wawekezaji gani watakidhi vigezo zitatangazwa hivi karibuni.

Tutazidi kukuletea taarifa hizi za uwekezaji kwa makampuni ya simu nchini.


COMMENTS

Name

kimataifa,1,Mlipuko,1,mtandao,1,teknolojia,1,
ltr
item
BONGO DONE: Sasa ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji
Sasa ni Rasmi Vodacom Tanzania Kuanza Kuuza Hisa Zake Kwa Wawekezaji
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhc0AnDRk-FmnBdCJK04aq46eQN9u5KBe3n1tWkb5pbAK2kgY0pP_LBXGA14jXFybgYp417cvKBzFokbMv_pzr4tcVYvzqAWl4z_a07_OJu_lL0fe85XFbjRauEqIjWz8CqWs7XnyRN7cuf/%20cursor:%20pointer;
BONGO DONE
https://bongodone.blogspot.com/2017/03/sasa-ni-rasmi-vodacom-tanzania-kuanza.html
https://bongodone.blogspot.com/
https://bongodone.blogspot.com/
https://bongodone.blogspot.com/2017/03/sasa-ni-rasmi-vodacom-tanzania-kuanza.html
true
5217992609549716446
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy